Rais wa Uchina Xi Jinping amekiri kwamba kirusi korona chaenea kwa kasi mno na sasa nchi inakumbwa na hali hatari
Kirusi Korona kimewauwa zaidi ya watu 56 na takriban watu 2, 000 wameambukizwa tangia mlipuko wa ugonjwa huo.
Ripoti zilizothibitiwa zinaarifu kwamba kesi 1,200 zimerokodiwa katika majimbo 29 nchini Uchina
Inaaminiwa kwamba chanzo cha mlipuko huo ni mji wa Wahun ambako mamia ya wafanyikazi wa afya wamepelekwa
Marekani sasa imetangaza kwamba itawaondoa wahudumu wake Wahun kupitia ndege maalum ili kuwasafirishwa had San Fransisco
Hata hivyo, watafiti ambao wana makao yao UK wameeleza hofu yao kwamba Uchina huenda ikashindwa kudhabiti kuenea kwa kirusi korona
Sasa hivi, vikwazo vya usafiri vimekumba miji mbali mbali nchini Uchina kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.
Vile vile, kirusi hicho kimeweza kuenea katika nchi nyingine kama vile Marekani, Ufaransa na Australia.
Uchina sasa inajenga hospitali ambayo itakayomudu vitanda 1000 ili kukumbana na kirusi hicho.
